Monday, January 09, 2012

Rais wa Guinea Bissau Malam Bacai Sanha Afariki Dunia

Aliyekuwa Raisi wa Guina Bissau Malam Bacai Sanha

Raisi wa Guinea Bissau Malam Bacai Sanha amefariki dunia mapema jumatatu hii, habari hizi zimetolewa na afisa wa balozi wa nchi za  Afrika ya Magharibi mjini Paris Ufaransa.
Habari zinadai kuwa Raisi Sanha alikmuwa Paris kwa matibabu ambapo umauti ulimkuta katika hospitali ya kieshi ya Val-de-Grace japo ugonjwa uliopelekea kifo chake haukuwekwa wazi kwa raia.

Sanha alichaguliwa kuwa Raisi mnamo mwezi Septemba 2009, mwezi mmoja baada yav kuuwawa aliyekuwa Raisi JOAO BERNARDO VIEIRA.
Hata hivyo nchi ya Guinea Bissau imekuwa ikikumbwa na mapinduzi ya kijeshi mara kwa mara tangu nchi hiyo ijipatie uhru waku kutoka katika ukoloni wa Wareno mwaka 1974 ambapo mapinduzi na vurugu hizo za kisiasa zimeuzorotesha kwa kiasi kikubwa uchumi wan chi hiyo pamoja na kuharibu miundombinu  yake jambon lililoipelekea nchi hiyo kuwa miongoni mwa nchi maskini sana duniani.
Mungu ailaze roho yake mahali pema poeponi

No comments:

Post a Comment